MAFAO

MAFAO YA URITHI

Penshen ya urith inalipwa kwa wategemezi wa mtumishi mwanachama wa TPF aliyepoteza uhai. Mafao ya urithi yamekusudiwa kufidia upotevu wa msaada wa kiuchumi uliokuwa ukitolewa na mtumishi aliyepoteza uhai.

Warithi
Warithi kwa mujibu wa mwongozo wa TPF ni mwenza na watoto ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 au 21 kama wanasoma shuleni au chuoni, au wazazi kama mtumishi hajaacha mwenza wala mtoto.

Masharti ya pensheni ya urithi

Pensheni ya urithi itatolewa kwa warithi kama mtumishi wakati anafariki:-

  1. Alikuwa na sifa za kupata pensheni ya uzee au
  2. Alikuwa na sifa ya kupata mafao ya ulemavu

Mafao yatakayolipwa

  • Kanuni ya kukokotoa pensheni ya uzee itatumika kukokotoa pensheni ya urithi
  • Pensheni inagawanywa kati ya mwenza na watoto, 40% ya pensheni atalipwa mwenza na 60% wanalipwa watoto. Kama hakuna mwenza wala watoto 100% ya penshen italipwa kwa wazazi wa marehemu.
  • Kwa mtumishi aliyekuwa ametimiza masharti ya pensheni ya urithi wategemezi wanapata malipo ya mkupuo wa awali na penshen ya kila mwezi
  • Kama mtumishi alikuwa ameanza kulipwa pensheni ya uzee au ulemavu mwenza ataendelea kulipwa 50% ya pensheni
  • Mkupuo maalum kama mtumishi alikuwa hajatimiza masharti ya pensheni ya urithi

Usimwache mwenzi na watoto wako bila uangalizi wa baadae