Pensheni ya Uzeeni

MAFAO YA UZEENI

Kusudi la msingi la pensheni ya uzee ni kumhakikishia usalama wa kipato mtumishi aliyeishiwa nguvu kwa sababu ya uzee. Mtumishi anapokea kipato kila mwezi

Masharti ya pensheni ya uzee

Pensheni inalipwa kwa mtumishi ambaye:

 1. Amefikisha angalau umri wa pensheni (miaka 70)
 2. Amefikisha umri wa miaka 65 au zaidi lakini chini ya umri wa pensheni
 3. Amekoma kuwa kwenye huduma wakati wote kwa sababu ya umri
 4. Amechangia angalau michango ya miezi 180.

Mwongozo wa Mfuko umetoa unafuu wa idadi ya michango kwa watumishi waliokuwa wamebakiza chini ya miaka 15 kufikia umri wa pensheni wakati Mfuko unaanza, yaani tarehe 1/1/2019. Watumishi watatimiza sifa za kupata pensheni kwa idadi ndogo ya michango kwa kuzingatia umri aliokuwa nao

Mafao yatakayolipwa

 • Malipo ya mkupuo wa awali, kabla ya kuanza kulipwa pensheni
 • Malipo ya mkupuo maalum kwa wale ambao hawajatimiza masharti, watarejeshewa michango yao na faida
 • Malipo ya pensheni ya kila mwezi

Kanuni ya kukokotoa (kikokotoo cha) pensheni ya uzee

Mtumishi atakayetimiza masharti atalipwa mkupuo wa awali na pensheni ya kila mwezi

 1. Mkupuo wa awali

CP = (1/580*N*APE) *12.5*25%


Tafsiri:-
 • CP = Malipo ya mkupuo
 • 1/580 = Kiwango cha fidia
 • N = Idadi ya michango
 • APE = Kipato cha mwaka - (APE ni wastani wa mapato ya miaka mitatu iliyokuwa na kipato kikubwa zaidi kati ya miaka 10 ya mwisho kabla yakutimiza umri wa penshen)
 • 12.5 = wastani wa miaka ya kulipwa pensheni (wastani wa umri wa kuishi baada ya kutimiza umri wa penshen)
 • 25% = Sehemu ya pensheni ya miaka 12.5 inayolipwa kwa mkupuo.

Malipo ya kila mwezi ya pensheni ya uzee

Pensheni ya kila mwezi = (1/580 * N*APE)*75%*1/12


Tafsiri:-

  1. 1/580 = Kiwango cha fidia
  2. N = Idadi ya michango
  3. APE = Kipato cha mwaka
  4. 75% = Sehemu ya pensheni ya mwaka baada ya malipo ya mkupuo ya 25%.

Say goodbye to tension and hello to your pension