Pensheni ya Ulemavu

MAFAO YA ULEMAVU

Penshen ya ulemavu inalipwa kwa mtumishi aliyepoteza uwezo wa kufanya kazi kwa sababu ya ulemavu wa kudumu uliosababishwa na ajali au ugonjwa

Masharti ya pensheni ya ulemavu

Pensheni ya ulemavu italipwa kwa mtumishi wa kanisa ambaye:-

  1. Amepata ulemavu wa kudumu.
  2. Yuko chini ya umri wa pensheni
  3. Amelipa michango ya miezi 180
  4. Amelipa angalau michango 36 na kati ya hiyo, michango angalau 12 imelipwa katika kipindi cha miezi 36 inayoishia tarehe ya kupata ulemavu.

Mafao yatakayotolewa

  • Kanuni ya kukokotoa mafao ya uzee itatumika isipokuwa idadi ya michango inaanzia 36.
  • Malipo ya mkupuo na pensheni ya kila mwezi.
  • Mkupuo maalum kwa mtumishi ambaye hatatimiza masharti, atarejeshewa michango na faida.

Katika hali yako, amini unaweza na Mungu atakuwezesha.